Ufadhili

Tunamshukuru sana Mungu kwa kukuwezesha kutembelea na kujifunza kupitia tovuti yetu. Tunaamini kuna jambo au mambo ambayo umejifunza ambayo yanaongeza kasi ya ukuaji wako katika imani ndani ya Kristo. Kwa kuwa tunaishi katika wakati ambapo maneno ya Mungu yanapaswa kufikia watu wengi zaidi kupitia njia za mitandao bila kikwazo cha gharama na sisi tuna nia ya kufanya hivyo kwa nguvu zaidi, tunapenda kukushirikisha uhitaji wetu.

Tovuti yetu inatoa nyenzo zote za kujifunza Biblia na kuhusu kanisa bila malipo ya aina yoyote. Hata hivyo, ni ukweli kwamba kuna gharama nyuma ya shughuli zetu zote. Hivyo, tunapenda kukukaribisha kutoa sadaka yako kwa ajili ya kuunga mkono kazi hii ili iweze kuendelea mbele.

Kazi yetu ni kutengeneza miongozo na fafanuzi za kila kitabu cha Biblia na kufundisha waamini historia ya kanisa kutoka karne ya kwanza mpaka sasa. Utimilifu wa kazi hii unahitaji rasilimali mbalimbali, kubwa ikiwa ni fedha. Kwa hivyo, tunakukaribisha kutoa kiasi chochote cha sadaka ambacho Bwana amekuwezesha kuwa nacho.

Sadaka zako zitatusaidia kulipa gharama za uendeshaji wa tovuti, kufanya utafiti wa kifundisho, na kuandaa maudhui ya maandishi, sauti, na video ambayo yatawasaidia waamini wengi kukua katika imani.

Unaweza kutoa sadaka yako kupitia njia zifuatazo

1. Kwa njia ya Simu - M-Pesa Tanzania

Nambari ya akaunti ya Mpesa Tanzania: +255 753 570 363
Jina la akaunti ya Mpesa Tanzania: Assa Smart Jotham

2. Kwa njia ya Benki - Access Bank Tanzania

Access Bank Tanzania
Nambari ya akaunti: 174 692 5114
Jina la akaunti: Assa Smart Jotham

Kama ungependa kujua bajeti yetu ya mwaka ili kuona jinsi unavyoweza kutoa kwa ajili ya kuunga mkono huduma hii, unaweza kutuandikia kupitia mawasiliano yetu hapo chini.

Wasilana Nasi

Tutafurahi Kusikia kwako. Tutumie ujumbe wako